100 集

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • 新聞

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu

    Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu

    Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Hafla hii pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. Wameketi na Flora Nducha na kumweleza walichoambulia hadi sasa katika jukwaa hilo litakalokunja jamvi kesho..

    • 8 分鐘
    Mapigano na mizozo DR Congo yanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao - Türk

    Mapigano na mizozo DR Congo yanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao - Türk

    Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
    Video ya Umoja wa Mataifa inaanzia Kinshasa mji mkuu wa DRC ambako Bwana Türk na aafisa mmoja wa Umoja wa Mataifa wanatazama ramani ya taifa hilo lililoko Maziwa Makuu na kisha anasema ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini tunaona ni kwa vipi utajiri huu kwa bahati mbayá hauko kunufaisha wananchi kwa sababu ya mapigano.
    Na kisha anaelezea mipango ya ziara yake ya kutathmini hali ya haki za binadamu akisemakwanza ni kukutana na watu waliofurushwa makwao kutokana na ghasia na vile vile kuonana na mamlaka husika na mashirika ya kiraia.
    Baada ya hapo safari inaanza akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, mwelekeo ni Mashariki mwa nchi jimboni Ituri. Taswira ya angani kutoka ndege hii ya Umoja wa Mataifa na kisha wanawasili. Mapokezi hapa Bunia, kutoka kwa wenyeji wao.
    Moja kwa moja msafara wao wa magari unafika kwenye kambi ya wakimbizi nje kidogo ya mji wa Bunia na wanaingia ndani ambako wanawake, wanaume na watoto, wazee na vijana, nyuso zao zinaonesha matuamini kwani wahenga walinena mgeni njoo mwenyeji apone.
    Mkalimani akamweleza Turk kuwa wanachosema maeneo yao yametawaliwa na waasi na hawawezi kurejea makwao.
    Na ndipo Kamishna huyu Mkuu wa Haki za Binadamu baada ya kuwasikiliza wakimbizi na kuzungumza nao akatoka nje na kusema, “Nimekutana na kundi la watu ambao wamefurushwa makwao kutokana na mauaji ya kikatili na ya kutisha yaliyotekelezwa kwenye makazi yao. Na wamekuweko hapa kwa miaka minne sasa. Tamanio lao kubwa kabisa ni kuweza kurejea makwao.”
    Kwa sasa kuna takribani watu milioni 1.8 waliofurushwa makwao jimboni Ituri kati ya wakimbizi wote wa ndani milioni 7.2 nchini kote DRC.
    Kesho Bwana Turk atakuwa na mazungumzo na Rais President Félix Tshisekedi na maafisa wengine wa serikali, Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na vyama vya siasa pamoja na watetezi wa haki za binadamu na kisha atazungumza na waandishi wa habari.
      

    • 2 分鐘
    17 APRILI 2024

    17 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jitihada za Umoja wa Mataifa za kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunaelekea nchini Madagascar, kulikoni?
    Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano.Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.  Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunakofanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukkwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania.Na mashinani tutakupeleka nchini Madagascar kusikia ujumbe kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, lakini kwanza ni makala.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

    • 13 分鐘
    Mkutano wa ufadhili wapata msaada wa fedha wa dola milioni 610 kwa ajili ya Ethiopia

    Mkutano wa ufadhili wapata msaada wa fedha wa dola milioni 610 kwa ajili ya Ethiopia

    Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana  mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.
    Mkutano huo uliolenga kukusanya dola bilioni 1 za kimarekani kwa ajili ya miezi mitano ijayo, ulikuwa umeandaliwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Ethiopia na Uingereza, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya kibinadamu.  
    Mara tu baada ya mkutano huo Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Joyce Msuya, aliwashukuru wafadhili hao na kusema kuwa huo ni mwanzo tu na matumaini ni kuendelea na kuongeza msaada kwa mwaka mzima.
    Dharura ya kibinadamu nchini Ethiopia imekuwa ikiongezeka kupitia mizunguko ya ukame na mafuriko, na migogoro. Ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo unatarajiwa kufikia kiwango cha juu kwa watu milioni 10.8 wakati wa msimu wa muwambo kati ya mwezi Julai na Septemba.
    Viwango vya utapiamlo katika sehemu za Afar, Amhara, Tigray na mikoa mingine vinatia wasiwasi mkubwa na vinaendelea kuwa vibaya zaidi. Wakati huo huo, migogoro katika Tigray na mikoa mingine imeharibu maelfu ya shule, vituo vya afya, mifumo ya maji na miundombinu mingine ya jamii.
    Mama huyu ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ni wa eneo la Afar, mashariki mwa Ethiopia ambako pia kumeathiriwa na mafuriko anapaza sauti akisema, “Ninataka kulea na kusomesha watoto wangu vizuri. Nawatakia watoto wangu mema.”
    Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu wanaunga mkono mwitikio wa kitaifa wa kuongeza msaada wa kuokoa maisha kwa watu milioni 15.5, na msaada wa chakula kwa watu milioni 10.4 nchini humo Ethiopia. Kwa mwaka mzima, ili mpango huo ufanikiwe unahitaji dola za Marekani bilioni 3.24.

    • 1 分鐘
    16 APRILI 2024

    16 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanzania, Abeida Rashid Abdallah anafafanua kwa nini Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Zanzibar ni chanda na pete.  Pia tunakuletea muhtasari ya habari na mashinani kama zifuatazo.
    Leo mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kuonya juu ya vita inayoendelea kukatili maisha ya watu Gaza, na kusambaratisha miundombinu yakitaja kuwa wanawake karibu 10,000 wamepoteza Maisha tangu vita kuanza miezi sita iliyopita huku mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila dakika 10.Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limeng’oa nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Matrekani likiwaleta maelfu ya vijana kutoka kila kona ya Dunia. Joramu Nkumbi ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo kutoka Tanzania na anafafanua wanachokijadili mwaka huu.  Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa shirikiana na mashirika mengine 48 ya kibinadamu, ya maendeleo na serikali wametoa ombi la haraka la dola milioni 112 ili kuwasaidia zaidi ya wahamiaji milioni 2.1 na jamii zinazowahifadhi. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji na jamii hizo ni katika njia za uhamiaji za Mashariki na Kusini zkijumuisha Djibouti, Ethiopia, Somalia, Yemen, Kenya na Tanzania.Na mashinani leo tunakwenda mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hususan jimboni Ituri ambako huko ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umechukua hatua kukabili mashambulizi kutoka waasi, mashambulizi ambayo kila uchao yanazidi kufurusha raia. Mzungumzaji wetu ni Luteni Kanali Mensah Kedagni, msemaji wa kijeshi wa MONUSCO.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 12 分鐘
    Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

    Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

    Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.

    • 3 分鐘

關於新聞的熱門 Podcast

Global News Podcast
BBC World Service
端聞 | 端傳媒新聞播客
端传媒音頻 | Initium Audio
Hong Kong Today
RTHK.HK
The Daily
The New York Times
晨早新聞天地
RTHK.HK
Bloomberg Daybreak: Asia Edition
Bloomberg

你可能也會喜歡

United Nations的更多節目

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
UN News - Global perspective Human stories
United Nations
The Lid is On
United Nations
ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain
United Nations
Interviews
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations